Ni nini imani ya Kanisa Katoliki kuhusu sakramenti ya Kipaimara?

Updated at: 2024-07-16 11:49:27 (8 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Sakramenti ya Kipaimara ni sakramenti ya tatu katika Kanisa Katoliki baada ya Sakramenti ya Ubatizo na Ekaristi. Ni sakramenti muhimu sana katika maisha ya Mkristo, kwa sababu inaweka muhuri wa Roho Mtakatifu na inapeana nguvu ya kushuhudia imani yetu kwa Yesu Kristo. Kwa hivyo, ni muhimu kujua imani ya Kanisa Katoliki kuhusu sakramenti hii.
Kanisa Katoliki linaamini kwamba sakramenti ya Kipaimara inaweka muhuri wa Roho Mtakatifu kwa Mkristo na inawapa nguvu kushuhudia imani yao kwa Kristo. Inafuatilia mfano wa Yesu mwenyewe aliyehitimu huduma yake kwa ubatizo wa Roho Mtakatifu (Mathayo 3:16, Marko 1:10, Luka 3:22).
Kupitia sakramenti ya Kipaimara, Mkristo anapokea nguvu ya kushuhudia imani yake kwa Kristo. Roho Mtakatifu anamwongoza, kumtia nguvu na kumwimarisha katika imani yake. Hii inampa Mkristo uwezo wa kuwa shahidi wa Kristo katika maisha yake na miongoni mwa watu wake.
Kufuatia mfano wa Yesu, Kanisa Katoliki linatambua sakramenti ya Kipaimara kama sehemu muhimu ya kujiunga na Kanisa. Ni kielelezo cha uhusiano wa kina wa Mkristo na Kristo, na pia ni kielelezo cha uhusiano wake na Kanisa.
Sakramenti ya Kipaimara pia inaunganishwa na Sakramenti ya Ubatizo kwa sababu inaendeleza kazi ya Roho Mtakatifu ambayo ilianza katika ubatizo. Kwa hivyo, Kanisa Katoliki linahimiza watu kukamilisha ubatizo wao kwa kupokea sakramenti ya Kipaimara.
Katika Catechism ya Kanisa Katoliki, tunaona kwamba sakramenti ya Kipaimara inathibitisha imani ya Mkristo na inaimarisha uhusiano wake na Kanisa. (CCC 1285). Ni sakramenti ya kudumu ambayo inatukumbusha jukumu letu la kushuhudia imani yetu kwa Kristo na kuhudumia Kanisa.
Kanisa Katoliki pia linatambua kuwa sakramenti ya Kipaimara inaunganisha Mkristo na washiriki wengine wa Kanisa. Ni kielelezo cha umoja wa kanisa na inawawezesha Wakristo kushiriki katika huduma ya Kanisa la Kristo.
Kwa kumalizia, Kanisa Katoliki linathamini sana sakramenti ya Kipaimara kama sehemu muhimu ya maisha ya Mkristo. Ni sakramenti ambayo inaweka muhuri wa Roho Mtakatifu na inawapa nguvu kushuhudia imani yao kwa Kristo. Kama Mkristo, ni muhimu kushiriki katika sakramenti hii na kuzingatia yale inayofundisha ili kuimarisha imani yetu.
Updated at: 2024-07-16 11:49:51 (8 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Updated at: 2024-07-16 11:49:39 (8 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Biblia imeandikwa na Mungu kupitia waandishi wanadamu kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu. Hivyo Biblia ni Neno la Mungu. Hivyo mwandishi wa Biblia ni Mungu kupitia wanadamu (God is the primary author of the Bible while human authors are secondary authors). Mungu aliwavuvia (inspiration by the Holy Spirit) waandishi wanadamu ili waweze kuandika kile tu ambacho Yeye (Mungu) alitaka kiandikwe kwa ajili ya wokovu wa wanadamu.
Updated at: 2024-07-16 11:49:46 (8 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Biblia imeandikwa na Mungu kupitia waandishi wanadamu kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu. Hivyo Biblia ni Neno la Mungu. Hivyo mwandishi wa Biblia ni Mungu kupitia wanadamu (God is the primary author of the Bible while human authors are secondary authors). Mungu aliwavuvia (inspiration by the Holy Spirit) waandishi wanadamu ili waweze kuandika kile tu ambacho Yeye (Mungu) alitaka kiandikwe kwa ajili ya wokovu wa wanadamu. Kusema kuwa Biblia imeandikwa na Mungu kupitia wanadamu haina maana ya kuandikwa kwa njia ya imla (dictation), kana kwamba Mungu anataja sentensi au neno na wao wanaandika. Hapana, pamoja na kuwavuvia Roho Mtakatifu, waandishi wanadamu walikuwa huru kutumia vipawa mbalimbali vya uandishi na mazingira yao ili kufikisha ujumbe ambao Mungu amewavuvia. Hivyo walikuwa “active writers of the Bible, and not passive writers.” Walitumia akili (reason), utashi (will), ujengaji picha (imagination) na vipawa vingine. Lakini vipawa hivi vyote vilikuwa chini ya maongozi ya Roho Mtakatifu ili kuwawezesha waandishi wa Biblia kufikisha ujumbe kwa ufasaha bila makosa.
Hivyo kuelewa kifungu au ujumbe wa Biblia ni lazima kujua yafuatayo:
Maana aliyokusudia mwandishi (the meaning of the human author)
Kusudi/malengo ya Roho Mtakatifu
Na kwa kuwa kwa mara ya kwanza Biblia waliandikiwa Wayahudi na waandishi wengi walikuwa Wayahudi, hivyo tunapaswa kujua yafuatayo ili kufasiri Biblia vizuri:
Tamaduni za Wayahudi
Historia ya Wayahudi
Mambo ya Kijografia
Namna yao ya uandishi n.k
Jambo muhimu kuelewa
Namba, wanyama, rangi, vitu, watu, maeneo, shughuli mbalimbali n.k vilikuwa na maana sana kwa Wayahudi na kwa Wakristo wa kwanza. Hivyo si ajabu kuona vimetajwa au kutumika katika Biblia.
Kabla ya kuzungumzia namba tuzungumzie baadhi ya vitu, rangi, watu au mahali kama vinavyoongelewa kwenye kitabu cha Ufunuo na sehemu nyingine za Biblia:
kwenye Ufu.12:1+ anamaanisha taifa au mji, na siyo mwanamke kama tunavyojua
neno pembe kwenye Ufu. 5:6; 12:3 linamaanisha “mamlaka”. Hata kwenye kiswahili mtu akiambiwa kuwa “ameota pembe” maana yake anajifanya kuwa ana mamlaka fulani na hivyo ana kiburi.
kwenye Ufu. 4:8; 12:14 linamaanisha uwezo wa kufika mahali pote (mobility).
kwenye Ufu. 1:16; 2:12,16) linamaanisha Neno la Mungu, ambalo lina hukumu na kuadhibu.
kwenye Ufu. 7:9 ni ishara ya ushindi.
kwenye Ufu. 2:10; 3:11 ni ishara ya utawala na ufalme.
kama lilivyotumika kwenye Ufu. 13:1; 21:1 linamaanisha sehemu ya uovu, chanzo cha machafuko na kifo.
rangi nyeupe inamaanisha furaha ya ushindi (Ufu. 1:14; 2:17)
rangi ya zambarau huashiria anasa, utajiri na ufalme (Ufu. 17:4; 18:12,16). Kwenye Yohane 19:2,5; Mk. 15:17 vazi la zambarau huashiria “ufalme”. Kwenye Lk. 16:19 vazi la zambarau la yule tajiri liliashiria “maisha ya anasa”.
rangi nyeusi iliashiria kifo (Ufu. 6:5,12).
Namba zilikuwa na maana sana kwa Wayahudi kwa sababu za kimazingira, kiuandishi na kilugha. Kila namba ilikuwa na maana. Hebu tutazame baadhi tu ya namba hizo:
Namba hizi kwa Wayahudi (kwenye Biblia) zinamaanisha ukamilifu au utimilifu wa jambo (perfection or completion). Kwa mfano katika Kiebrania (lugha ya Wayahudi) hakuna “superlative” (kulinganisha kwa kutumia sifa ya juu kabisa) mfano “the tallest, the youngest, the holiest” kama kwenye Kiingereza. Hivyo Myahudi kwa upande wake atatamka neno husika mara tatu kuonesha ukamilifu: God is holy, holy, holy (ambapo kwenye Kiingereza tungesema tu “God is the holiest”). Kwa hiyo akitaja neno mara tatu alimaanisha ukamilifu wa jambo(perfection). Anaposema Mungu ni Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu ana maana kwamba Mungu ana ukamilifu wa utakatifu, yaani ni Mtakatifu kupita viumbe au vitu vyote. Mfano mwingine: Myahudi akisema kwamba nilipigwa viboko vitatu haina maana kuwa lazima vilikuwa vitatu tu. Hapa ina maana kwamba alipigwa katika ukamilifu wake yaani alipigwa barabara, sawia, alipigwa mno,
alipigwa mpaka basi. Hata kwenye Biblia ni vivyo hivyo. Yesu alimuuliza Petro mara tatu kama anampenda (Yohane 21:15-19). Hapa Yesu alitaka kujua kama Petro alimpenda katika ukamilifu wa upendo. Namba 7 imetumika mara 42 kwenye kitabu cha Daniel na Ufunuo: mfano “roho saba” ilimaanisha “ukamilifu wa roho” yaani Roho Mtakatifu. Kwa hiyo namba 3 na7 ni namba za ukamilifu. Yesu anapomwambia Petro asamehe “saba mara sabini” (Mt. 18:21-22) anamaanisha kuwa Petro asamehe “kwa ukamilifu, pasipo kukoma”.
Namba 4 kwenye Biblia inamaanisha “ulimwengu mzima” (universality of the visible world). Kwa hiyo aya isemayo “malaika wanne waliokuwa wamesimama katika pembe nne za dunia” (Ufu.7:1; 21:16; Rejea pia Is.11:12) ulimaanisha malaika walikuwa wameenea katika ulimwengu mzima. Pia aya hiyo hiyo inamaanisha kuwa jukumu lao lilikuwa ni kwa ulimwengu mzima.
Hii namba inasimama kumaanisha “mapungufu, isiyo kamilifu”. Namba hii ilihusianishwa na maadui wa Mungu kwenye Biblia. Kitendo cha mtu kuwa adui wa Mungu kilimaanisha mtu huyo si mkamilifu na ana mapungufu (Rejea 1 Nyakati 20:6; Daniel 3:1; Ufu.13:18).
Hizi mara nyingi kwenye Biblia zinawakilisha kabila kumi na mbili za Israeli. Wapo wataalam wa Maandiko wanaosema kuwa Mitume 12 waliwakilisha makabila 12 ya Israel, yaani kila mmoja alitoka miongoni mwa makabila 12 ya Israel. Pia namba 12 inawakilisha Kanisa zima. Lakini pia 12 ni namba ya ukamilifu. Kwa hiyo Mitume 12 walikamilisha taifa zima la Israeli.
Namba hizi kwenye Biblia zinamaanisha “urefu wa jambo” (longevity). Mfano wakisema fulani amekuwa mgonjwa kwa siku 40 ina maana amekuwa mgonjwa kwa kipindi kirefu, haina maana kuwa ni lazima zilikuwa 40 (huenda hata zilizidi). Kusema kuwa gharika ilidumu siku 40 mchana na usiku, ni kusema kuwa gharika ilidumu kwa kipindi kirefu; kusema kuwa Yesu alifunga siku 40 ni kumaanisha kuwa alifunga kwa muda au kipindi kirefu, yawezekana hata zaidi ya siku hizo 40. Kusema kuwa Waisraeli walikaa jangwani miaka 40 ni kusema kuwa walikaa jangwani kwa kipindi kirefu. Kusema kuwa Ibrahimu aliishi miaka 175 ina maana aliishi miaka mingi au kipindi kirefu, si lazima kwamba alifikisha miaka 175 lakini kwamba aliishi miaka ya kutosha, aliishi kipindi kirefu. Haya yote Wayahudi walielewa vizuri, hawakuhitaji kuuliza.
Kwenye Biblia ikitajwa namba ya maelfu inamaanisha “umati mkubwa” wa watu. Yohane anaposema “…na watu mia na arobaini na nne elfu pamoja naye..” (Ufunuo 14: 1) anamaanisha kuwa aliona umati mkubwa wa watu wasio na idadi. Hivyo Ufunuo 14:1 haimaanishi watu 144,000 tu bali umati mkubwa wa watu wasio na idadi. Hata kwa Kiswahili kuna wakati tunasema “akihubutia maelfu ya watu” tukiwa na maana kwamba alihutubia umati mkubwa wa watu.
N.B. Hapa nimeeleza baadhi ya namba tu. Zipo nyingine nyingi sana na zina maana yake. Hivyo tusitafsiri Biblia kwa maana sisisi tu (Literal interpretation), yaani kile kilichoandikwa tu. Twende zaidi ya hapo.
Kuelewa maana ya namba hii ni lazima kuelewa mazingira na sababu za kuandikwa kitabu cha Ufunuo. Kitabu cha Ufunuo kiliandikwa karne ya kwanza (kati ya 90-96 AD) ambapo dini ya Ukristo ilianza kuenea kwa kasi. Hivyo tawala za Warumi na Wayahudi ziliona Ukristo kama dini mpya na tishio kwa imani, siasa na tamaduni zao. Ili kuifutilia mbali Warumi na hata Wayahudi waliendesha madhulumu (persecutions) dhidi ya Wakristo: kuwaua, kuwafunga, kuwatesa na kuwalazimisha wakane Ukristo. Yohane mwenyewe anaandika kitabu cha Ufunuo akiwa gerezani (uhamishoni) katika kisiwa cha Patmos kama matokeo ya madhulumu. Yohane anaandika kitabu cha Ufunuo kuwatia moyo Wakristo katika madhulumu wanayopata, wasikate tamaa, wasikane imani kwa kuwa baada ya madhulumu watapata utukufu katika Yerusalem mpya (mbinguni) na damu watakayomwaga katika madhulumu ndiyo itawatakasa (Ufu. 7:14).
Kwa kuwa madhulumu yalikuwepo ilikuwa ni vigumu Wakristo kuwasiliana kwa lugha ya wazi ili kuepuka kuuawa au kufungwa. Hivyo Wakristo walitumia lugha ya namba na mafumbo kufikishiana ujumbe kwa waandishi (they used coded language). Kumtaja mfalme wa dola ya Kirumi kwa jina ilikuwa ni dharau na hivyo sababu tosha ya kuuawa. Yohane anatumia lugha ya namba kumtaja mmoja wa wafalme wakatili wa dola ya Kirumi aitwaye NERO kwa kutumia namba 666. Wakristo na wataalamu wa Maandiko Matakatifu walijuaje kuwa 666 inamwakilisha mfalme NERO? Mpaka leo kwa Warumi na Wagiriki kila herufi imepewa thamani ya namba. Walipojumlisha herufi zinazounda jina “NERO” walipata jumla ya 666. Kwa Warumi jina la NERO liliandikwa NERON (likiwa na “N” mwishoni). Walijumlisha herufi za jina NERON na kupata 666 na hivyo kugundua kuwa mnyama aliyetajwa kwenye Ufu. 13:11-18 alikuwa NERO. Kwa nini amezungumziwa mnyama halafu sisi tunazungumzia mtu? Ni kwa sababu Yohane mwenyewe anasema: “Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu [for it is man's number]. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita” (Ufu. 13:18).
Utaalamu wa kuzipa herufi thamani ya namba unaitwa “gematria”. Mfumo wa kuzipa herufi thamani ya namba unafanana na kutofautiana kwa kiasi fulani kwa Warumi na Wagiriki. Utaratibu wa kuthaminisha herufi na namba upo bado. Ndiyo maana tukiwa shule ya msingi tulifundishwa “Namba za Kirumi”. Tunajuaje kuwa MM ni 2000 au MMIX ni 2009. Ni kwa sababu kwa Warumi kila herufi ina thamani ya namba: M ni 1000, hivyo M+M ni sawa na kusema 1000+1000, na hivyo 2000. Tuone sasa kwa jina NERO na thamani ya kila herufi.
Gematria kwa Kirumi: NERON
N = 50
E = 6
R = 500
O = 60
N = 50
neron (50 + 6 + 500 + 60 + 50) = 666
Wayunani walitamka jina ya mfalme kwa kuanza na jina la heshima “title” yaani Kaisari (Ceaser). Hivyo NERO aliitwa qsr nrwn (Kaiser Neron, kwa Kigiriki). Mwanzoni Kiebrania (Kiyunani) hakikuwa na irabu (vowels). Herufi zilizounda neno qsr nrwn (Kaiser Neron) zilipewa thamani ya namba kama ifuatavyo:
q = 60
s = 100
r = 200
n = 50
w = 6
Hivyo basi neno qsr nrwn (60 + 100 + 200 + 50 + 200 + 6 + 50) = 666.
Na Fr. Kelvin O. Mkama
Updated at: 2024-07-16 11:49:41 (8 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
26 Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya, 27 kwa msichana mmoja aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi. 28 Malaika akamwendea, akamwambia, "Salamu Maria! Umejaliwa neema nyingi! Bwana yu pamoja nawe." 29 Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: maneno haya yanamaanisha nini? 30 Malaika akamwambia, "Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema. 31 Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume na utampa jina Yesu. 32 Yeye atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu. Bwana Mungu atampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake. 33 Kwa hivyo atautawala ukoo wa Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho." 34 Maria akamjibu, "Yatawezekanaje hayo, hali mimi ni bikira?" 35 Malaika akamjibu, "Roho Mtakatifu atakushukia, na uwezo wake Mungu Mkuu utakujia kama kivuli; kwa sababu hiyo, mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu. (Luka 1:26-35)
19 Baada ya kifo cha Herode, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto kule Misri, 20 akamwambia, "Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, urudi tena katika nchi ya Israeli, maana wale waliotaka kumwua mtoto huyo wamekwisha kufa." 21 Basi, Yosefu aliamka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, akarejea katika nchi ya Israeli. 22 Lakini Yosefu aliposikia kwamba Arkelao mwanawe Herode alikuwa mfalme wa Yudea mahali pa baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye baada ya kuonywa katika ndoto, alikwenda katika mkoa wa Galilaya, 23 akahamia katika mji uitwao Nazareti. Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyonenwa kwa njia ya manabii: "Ataitwa Mnazare." Matayo 2:19-23
41 Wazazi wa Yesu walikuwa na desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka wakati wa sikukuu ya Pasaka. 42 Mtoto alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, wote walikwenda kwenye sikukuu hiyo kama ilivyokuwa desturi. 43 Baada ya sikukuu, walianza safari ya kurudi makwao, lakini Yesu alibaki Yerusalemu bila wazazi wake kuwa na habari. 44 Walidhani alikuwa pamoja na kundi la wasafiri, wakaenda mwendo wa kutwa, halafu wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa na marafiki. 45 Kwa kuwa hawakumwona, walirudi Yerusalemu wakimtafuta. 46 Siku ya tatu walimkuta Hekaluni kati ya walimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. 47 Wote waliosikia maneno yake walistaajabia akili yake na majibu yake ya hekima. 48 Wazazi wake walipomwona walishangaa. Maria, mama yake, akamwuliza, "Mwanangu, kwa nini umetutenda hivyo? Baba yako na mimi tumekuwa tukikutafuta kwa huzuni." 49 Yeye akawajibu, "Kwa nini mlinitafuta? Hamkujua kwamba inanipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu?" 50 Lakini wazazi wake hawakuelewa maana ya maneno aliyowaambia. 51 Basi, akarudi pamoja nao hadi Nazareti, akawa anawatii. Mama yake akaweka mambo hayo yote moyoni mwake. 52 Naye Yesu akaendelea kukua katika hekima na kimo; akazidi kupendwa na Mungu na watu. (Luka 2:41-52).
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?" (Mathayo 13:55-56)
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?" (Mathayo 13:55-56)
35 Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo, walimwendea Yesu wakamwambia, "Mwalimu, tunataka utufanyie kitu tutakachokuomba." (Marko 10:35)
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56)
19 Lakini sikuwaona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana. (Wagalatia 1:19)
1 Mimi Yuda, mtumishi wa Yesu Kristo, ndugu yake Yakobo, nawaandikia ninyi mlioitwa na Mungu na ambao mnaishi katika upendo wa Mungu Baba, na katika ulinzi wa Yesu Kristo. (Yuda 1:1)
25 Karibu na msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mama yake, na dada ya mama yake, Maria mke wa Kleopa, na Maria Magdalene. (Yohana 19:25)
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56).
26 Yesu alipomwona mama yake, na karibu naye amesimama yule mwanafunzi aliyempenda, akamwambia mama yake: "Mama! Tazama, huyo ndiye mwanao." 27 Halafu akamwambia yule mwanafunzi: "Tazama, huyo ndiye mama yako." Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake.
Updated at: 2024-07-16 11:49:13 (8 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Kanisa Katoliki linatambua kuwa Mungu aliumba ulimwengu na binadamu kwa mapenzi yake, lakini pia Mungu alitupa uhuru wa kuchagua. Ni wajibu wa binadamu kutimiza matakwa ya Mungu na kuishi maisha yanayoambatana na mapenzi yake.
Katika Waraka wa Yohane Paulo II, Fides et Ratio, Kanisa Katoliki linatilia mkazo kwamba binadamu ana jukumu la kutafuta ukweli na kuelewa mapenzi ya Mungu. Kupitia kwa imani na akili, binadamu anaweza kufikia maarifa ya ukweli huu.
Katika Maandiko Matakatifu, tunaona jinsi ambavyo Mungu anatutaka kufuata mapenzi yake. Mtume Paulo aliandika katika Waraka wa Waebrania 10:36, "Kwa hiyo, ninyi mnahitaji subira ili mtimize mapenzi ya Mungu na mpokee ahadi yake." Hii inamaanisha kuwa kwa kumtii Mungu na kufuata mapenzi yake, tunaweza kufikia ahadi zake.
Kanisa Katoliki linamfundisha mtu anapaswa kumtii Mungu na kusubiri mapenzi yake. Hii inamaanisha kuwa tunapaswa kufuata amri za Mungu na kuishi maisha yenye haki na kwa upendo. Katika KKK 2822, inasemekana, "Tunatafuta mapenzi ya Mungu katika maisha yote, hasa katika maamuzi yetu muhimu."
Katika Maandiko Matakatifu, tunajifunza kwamba Mungu anataka tufanye kazi yetu kwa bidii na kwa upendo. Paulo aliandika katika Waraka wa Wakolosai 3:23-24, "Kila mfanyalo, fanyeni kwa moyo wenu wote, kama kwa Bwana, si kwa ajili ya wanadamu, kwa maana mnajua ya kuwa mtapokea ujira wa mrithi kutoka kwa Bwana."
Kanisa Katoliki linatilia mkazo kwamba inatupasa kufanya kazi kwa heshima na kwa uaminifu, kwa kuwa kwa kufanya hivyo tunamfurahisha Mungu. Kanuni ya Maadili ya Kikatoliki inatufundisha kuwa tunapaswa kutoa kazi yetu kwa Mungu na kuifanya kwa uangalifu na upendo, ili kuonyesha upendo wetu kwa Mungu.
Kwa hiyo, Kanisa Katoliki linatambua kwamba tunapaswa kutimiza matakwa ya Mungu na kuishi maisha yanayoambatana na mapenzi yake. Tunapaswa kumtii Mungu, kufanya kazi yetu kwa bidii na kwa upendo, na kutafuta ukweli na maarifa ya mapenzi yake. Kwa kufanya hivyo, tunapata baraka za Mungu na kupokea ujira wake wa milele.
Updated at: 2024-07-16 11:49:12 (8 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Je, Kanisa Katoliki linawahimiza waamini kuishi uadilifu wa kijamii na kupinga ubaguzi na ukosefu wa haki katika jamii? Jibu ni ndiyo! Kanisa Katoliki linaamini kuwa uadilifu wa kijamii na kupinga ubaguzi na ukosefu wa haki ni sehemu muhimu ya imani ya Kikristo. Kama Wakatoliki, tunapaswa kuishi kwa mfano wa Yesu Kristo, ambaye alikuwa mshikamano na watu wote, na aliwajali wote bila ubaguzi.
Kwa mujibu wa Catechism ya Kanisa Katoliki, kila mtu ni mwenye heshima kwa sababu yeye ni waumba wa Mungu. Kwa hiyo, tunapaswa kuwatendea wote kwa heshima na upendo. Hii inamaanisha kwamba hatupaswi kuwabagua watu kwa msingi wa jinsia zao, rangi ya ngozi, au hali yao ya kiuchumi. Badala yake, tunapaswa kuwajali wote, na kuwapa haki sawa, upendo, na msaada wanaohitaji.
Bible inakumbusha kwetu kuwa "Basi, kwa sababu ya hili, ni lazima kumtii mtawala, si kwa sababu ya adhabu tu, bali kwa sababu ya dhamiri yako pia. Kwa sababu hii pia mliwalipa kodi; kwa kuwa wao ni wahudumu wa Mungu, wakishughulikia kazi yao kwa bidii. Mlipeni kila mtu kodi yake; yeye ambaye kodi, kodi; yeye ambaye ushuru, ushuru; yeye ambaye hofu, hofu; yeye ambaye heshima, heshima" (Warumi 13:5-7). Kwa kufuata kanuni hizi, tunaweza kuishi kwa amani na kwa kufurahia maisha mema na mazuri.
Kanisa Katoliki pia linatuhimiza kupinga ubaguzi na ukosefu wa haki. Kwa mujibu wa Catechism, "ubaguzi ndio upinzani wa Mungu kwa sababu ni kukiuka heshima ya watu wengine kama waumba wa Mungu" (CCC1935). Tunapaswa kushughulikia ubaguzi katika jamii kwa kuelewa kuwa ubaguzi una madhara makubwa kwa watu binafsi na jamii kwa ujumla.
Kama Wakatoliki tunafundishwa kupigana dhidi ya ubaguzi na ukosefu wa haki. Biblia inatufundisha kuwa "Mungu hana upendeleo" (Matendo ya Mitume 10:34), na tunapaswa kuishi kwa mfano wa Kristo, ambaye alikuwa mshikamano na watu wote, bila ubaguzi. Hii inamaanisha kwamba tunapaswa kupinga ubaguzi wa aina yoyote, iwe ni ubaguzi wa rangi, jinsia, kabila, au hali ya kiuchumi.
Kwa ufupi, Kanisa Katoliki linawaalika waamini wake kuishi kwa uadilifu wa kijamii na kupinga ubaguzi na ukosefu wa haki katika jamii. Tunapaswa kuishi kwa mfano wa Kristo, ambaye alikuwa mshikamano na watu wote, na aliwajali bila ubaguzi. Kwa kufuata kanuni hizi, tunaweza kuishi kwa amani na kwa kufurahia maisha mema na mazuri.
Updated at: 2024-07-16 11:49:49 (8 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
KALENDA za mwanzo ziliutumia mwezi wa
angani kama kipimo cha muda. Ziliitwa
“Lunar calender” au Kalenda-Mwezi. Tarehe 1
ya Mwezi ilikuwa ni siku ulipoandama yaani
Mwezi-Mdogo (Crescent Moon).
Mwezi unapofika siku ya 15 unakuwa
umefikia ukubwa wa juu na huitwa Mwezi-
Mkubwa (Full Moon). Hivyo kwa kalenda ile
tarehe 15 ilikuwa ni siku ya Mwezi-Mkubwa.
Mwaka 45KK, Julius Caesar alitangaza
kalenda mpya ikaitwa “Julian Calender” iwe
na siku 365. Wakati huo ikijulikana kwamba
jua huzunguka kwa siku 365.25. Hivyo pengo
la kalenda na mzunguko likabaki robo siku.
Updated at: 2024-07-16 11:49:43 (8 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
KALENDA za mwanzo ziliutumia mwezi wa angani kama kipimo cha muda. Ziliitwa “Lunar calender” au Kalenda-Mwezi. Tarehe 1 ya Mwezi ilikuwa ni siku ulipoandama yaani Mwezi-Mdogo (Crescent Moon). Mwezi unapofika siku ya 15 unakuwa umefikia ukubwa wa juu na huitwa Mwezi- Mkubwa (Full Moon). Hivyo kwa kalenda ile tarehe 15 ilikuwa ni siku ya Mwezi-Mkubwa. Mwaka 45KK, Julius Caesar alitangaza kalenda mpya ikaitwa “Julian Calender” iwe na siku 365. Wakati huo ikijulikana kwamba jua huzunguka kwa siku 365.25. Hivyo pengo la kalenda na mzunguko likabaki robo siku. Robo hiyo ifidiwe kila baada ya miaka minne mwishoni mwa mwezi Februari ambayo sasa ulifanywa kuwa wa pili baada ya January. Inapofanyika hivyo, huo ukaitwa mwaka- mrefu (Leap year). Mwaka mrefu ukachaguliwa kuwa ni ule tu unaogawanywa kwa nne mfano miaka ifuatayo 1700, 1800, 1900, 2100, 2200, 2300. Baadaye iligundulika kuwa jua huzunguka kwa siku 365.24218967 ziitwazo “Tropical year”. Hizi ni chache kuliko siku 365.25 zilizokadiriwa mwanzoni. Uchache huu husababisha kuwe na pengo la dakika 11 na sekunde 14.812512 kwa mwaka. Pengo hili ni dogo, lakini hupanuka hadi kuwa siku nzima kila baada ya miaka 128.0355. Mwaka 1545 lilivuka siku 9.25. Kuondoa tatizo hili, Papa Gregory XIII aliamuru iundwe kalenda mpya na akachagua Oktoba 04, 1582 iwe siku ya mwisho kutumika “Julian Calender”. Kesho yake, kalenda mpya ikaanza kutumika. Ungetegemea hiyo kesho iwe ni Oktoba 05, 1582. Lakini ili uzibe pengo lile lililofikia siku kumi, ilibidi kalenda mpya kuziruka siku hizo siku kumi. Hivyo hii mpya iliyoitwa “Gregorean Calender” ikaanza kama Oktoba 15 badala ya Oktoba 05. Ndiyo sababu katika historia ya nchi nyingi Ulaya, hakuna tarehe za Oktoba 05, 1582 hadi Oktoba 14, 1582. Watu walilala Oktoba 04, 1582 kesho yake wakaamka ikiwa ni Oktoba 15, 1582. Teresa Alonso huandikwa kwamba alifariki Oktoba 1582, kwenye usiku wa tarehe NNE kuamkia tarehe KUMI NA TANO! Alipotangazwa kuwa Mtakatifu, Kanisa Katoliki likaifanya Oktoba 15 kuwa siku ya kumkumbuka, yaani siku ya Mtakatifu Teresa wa Avila. Usipofahamu kwamba Mtakatifu Teresa alifariki siku kalenda zinabadilishwa, utadhani aliyeandika vile tarehe za kifo chake amekosea! Waandishi, William Shakespeare wa Uingereza na Miguel de Cervantes wa Spain huandikwa kwamba wote walifariki Aprili 23, 1616. Lakini ukweli ni kwamba hawakufa siku moja bali walipishana siku kumi kwani England ilichelewa kwa karibu miaka 200 kuikubali “Gregorean Calender”! “Gregorean Calender” haikuundwa ili kuishia kuliziba lile pengo. Bali pia, kuhakikisha halitokei tena. Tumeshaona kuwa lile pengo ni dakika 11 na sekunde 14.812512. Hivyo, linapanuka na kuwa siku tatu ndani ya miaka 400. Hivyo kuliziba inatakiwa kupunguza siku tatu kila baada ya miaka 400.Kijana mmoja alisafiri kwa meli na rafiki zake,
wakiwa katikati ya safari yao meli ilianza
kuzama. Watu wengi pamoja na rafiki wa yule
kijana walikufa maji wakati wanajaribu kujiokoa
kwa kuogelea, lakini yule kijana alifanikiwa
Updated at: 2024-07-16 11:49:45 (8 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Kijana mmoja alisafiri kwa meli na rafiki zake,
wakiwa katikati ya safari yao meli ilianza
kuzama. Watu wengi pamoja na rafiki wa yule
kijana walikufa maji wakati wanajaribu kujiokoa
kwa kuogelea, lakini yule kijana alifanikiwa
kushika ubao ulioelea majini akaanza kuelea nao,
maji yalimpeleka hadi kisiwa cha mbali sana
ambako hakukuwa na watu wala wanyama
isipokuwa wadudu tu! Alifika ufukweni amechoka
sana na asiyeamini tukio lililotokea, akaishi huko
kwa kula matunda. Aliweza kujenga ka-kibanda
kwa shida sana maana hakuwa na shoka wala
panga, hatimaye akaanza maisha mapya.
Aliishi muda mrefu kisiwani na tayari alishazoea
mazingira yale ya shida japo shida haizoeleki.
Mara zote nyakati za jioni aliwasha moto kwa
kupekecha vijiti. Siku moja kama kawaida yake
aliwasha moto nje karibu na kibanda chake, aliota
moto muda mrefu hatimaye akapitiwa na usingizi.
Alilala hapo hapo hadi usiku wa manane
aliposhtushwa na joto kali lisilo la kawaida.
Kumbe moto ulishika nyasi za kibanda chake na
kibanda chote kikaungua moto.Alilia sana na
kumlaani sana Mungu kwa mateso hayo akisema
"Hivi Mungu nimekukosea nini mpaka unitese
hivi? Pamoja na shida zote hizi bado
unaniongezea shida nyingine, umeteketeza makazi
yangu ilhali nimejenga kwa shida, Hukuridhika
kunitenga mbali na familia yangu nilipoishi kwa
raha? Hukuridhika kuwaua rafiki zangu wote
baharini? Kwanini Mungu umekuwa mkatili hivi?
Bora nife tuu maana nimeshachoshwa na hizi
shida!" akaendelea kulalamika na kumlaani Mungu
hadi kukapambazuka.
Ilipofika asubuhi aliiona meli ikija kwa mbali
kuelekea alipo, alishangaa maana hakuna meli
yoyote inayoweza kwenda kisiwa kile labda kama
imepotea njia. Meli ilipofika ufukweni yule kijana
akaifuata, alienda moja kwa moja hadi kwa
kapteni.Kapteni akamwambia "tuliona moto mkali
sana usiku tukahisi ni meli inawaka moto
tukasema tuje ili tutoe msaada..kwa kweli
tumetembea masaa mengi sana hadi kufika hapa,
mshukuru Mungu maana ametumia moto kutuleta
hapa" yule kijana kusikia hivyo alilia sana,
akajilaumu kwa jinsi alivyo mnung'unikia Mungu.
Akaelewa kuwa Mungu ana njia nyingi za kuleta
msaada kwa mtu. Akapiga magoti akatubu huku
akimshukuru Mungu. Safari ya kurudi nyumbani
ikaanza.
FUNDISHO: Wakati mwingine Kuna mambo
mabaya huwa yanatokea katika maisha yetu
yanayotufanya tuone kama Mungu ametusahau.
Tunamnung'unikia na kumlaumu Mungu bila
kujua kuwa Mungu ana njia nyingi sana kutuletea
msaada. Njia za Mungu huwa zinaonekana kama
ujinga fulani, lakini kiukweli ujinga wa Mungu
ndiyo akili kubwa ya mwisho ya mwanadamu.
Tunasahau kuwa mabaya tunayokutana nayo
yanafanya kazi kwa Manufaa ya hatma zetu.
Unaweza fukuzwa kazi usijue kumbe ndio
unaelekea katika kazi bora zaidi, unaweza
kuachwa na mtu uliyempenda sana ukadhani
ndiyo mwisho wa maisha kumbe Mungu
amekuandalia mtu mwingine mwenye mapenzi ya
dhati mtakayefikia malengo ya kujenga familia,
unaweza kukataliwa na kutengwa na ndugu
kumbe Mungu amekuandalia watu-baki
watakaofanikisha ufikie malengo yako pasipo
masimango ya ndugu, hata rafiki wanaweza
kukusaliti kumbe Mungu amewaondoa makusudi
ili kukuepusha na mabaya waliyoyapanga juu
yako. Sasa usimlaumu Mungu ukadhani
anakuzidishia matatizo, hapo anatafuta njia ya
kuyaondoa hayo matatizo.
Mshukuru Mungu kwa Kila Jambo, kwakuwa
hajawahi kukuwazia mabaya. Anakuwazia mema
sikuzote.
Tafadhari Share kama umeipenda na marafiki
zako wajifunze…….