Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Unganisha imani na maisha yako kupitia π Sala, π Masomo ya Misa, π Mafundisho, π‘ Tafakari, π° Makala, na π My System kwa usimamizi wa maisha binafsi. Tunakukaribisha kwenye safari ya kiroho na kimwili!.
Updated at: 2024-05-27 07:11:44 (10 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Upendo hauandamani na ubinafsi. Huwezi kusema una upendo wa kweli kama huwezi kujinyima vile unavyovipenda kwa ajili ya yule au wale unaowapenda. Upendo wa kweli ni kujitoa.
Updated at: 2024-05-27 07:11:47 (10 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Inashangaza kwa sasa watu wengi hawapendi kuambiwa kuhusu kutubu dhambi zao bali wanataka waambiwe watabarikiwa. Kama vile wewe huwezi kumvika mwanao nguo nzuri kabla ya kumuogesha vivyo hivyo na Mungu hawezi kukubariki kabla ya kukutakasa. Unapotubu unasamehewa na kutakaswa dhambi zako kisha unakua umefungua milango ya baraka. Huwezi kubarikiwa bila kutubu kweli.
Updated at: 2024-05-27 07:11:58 (10 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Sala pasipo Imani thabiti, ya nia ya kweli, upendo wa kweli, unyenyekevu wa ndani na tumaini la kweli katika Amani ya rohoni; Haijakamilika na haifai kitu.
Updated at: 2024-05-27 07:11:43 (10 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Usiache kusali na kutenda mema kwa kuwa huwezi jua ni watu wangapi wanategemea sala na matendo yako mema. Kumbuka Mungu alimwambia Abraham kama akikuta Wacha Mungu wengi hataiharibu Sodoma na Gomora. Vivyo hivyo Inawezekana wapo watu wengi wanaonufaika na Sala na matendo yako, hasa watu wako wa karibu uwapendao. Unapokuwa mtu wa Sala na mcha Mungu unabarikiwa wewe na wale wa karibu yako. KAMWE USIACHE KUMCHA MUNGU NA KUSALI. Ukiwa mregevu ni sawa na unakata Mnyororo wa Baraka za Mungu kwako na wenzako.
Updated at: 2024-05-27 07:11:42 (10 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Upendo wa kweli hauambatani na chuki. Huwezi kusema una Upendo wakati kuna watu wengine unawapenda na wengine unawachukia. Ni sawa na kusema kitambaa ni cheupe lakini kina madoa doa, maana yake sio cheupe.
Updated at: 2024-05-27 07:11:50 (10 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Usiogope wala usisite kutubu na kuomba msamaha kwa Mungu. Uwe na Amani na Matumaini katika Huruma ya Mungu itokayo katika Upendo wake wa Mfano wa baba awapendavyo wanawe. Mungu anasubiri kukupokea kwenye mikono yake Ili akutunze kama mtoto wake kama utatubu na kumrudia yeye. Amua kumwendea leo! Anakungoja ni wewe tuuβ¦