Mambo ya kufahamu kuhusu kuweka Tumaini kwa Mungu

Mtumainie Mungu kwa maana Mungu hawatupi wale wamtumainiao na kumgoja. Mkono wake upo tayari kwa ajili ya kuwaokoa wale wanaomwelekea.

Mpendwa Msomaji, Mtumainie Mungu kwa kila ufanyacho. Tumainia msaada na Baraka ya Mungu kwenye kila kitu katika maisha

Mungu yupo kwa Ajili yako

Mungu yupo kwa ajili ya;

 1. Kukupa nguvu na uwezo wa kufanya mambo yako yote vile inavyotakiwa.
 2. Kuibariki kazi ya Mikono yako
 3. Kukusaidia wewe usipatwe na matatizo
 4. Kukuokoa wewe katika matatizo yako
 5. Kukufariji katika magumu yako

Tumaini kwa Mungu

 1. Weka tumaini lako kwake kwa kumshirikisha kila kitu
 2. Anza na Mungu kwenye kila kitu
 3. Endelea na Mungu hata wakati unafanya jambo lolote
 4. Maliza na Mungu kwa kushukuru na kumpa utukufu
 5. Kwa kusema Yote yafanyike kwa Mapenzi yake

Utayari wa Mungu

Mungu yupo tayari;

 1. Kukupa nguvu na uwezo kuyafanya yote kwa kiwango kinachotakiwa
 2. Kukusaidia unaposhindwa kabisa
 3. Kulinda na kutunza kile unachokifanya
 4. Kukuokoa na chochote kile.

TAZAMA: Ni vyema na inaleta amani kufanya kila kitu kwa kumtegemea Mungu. 

 

NAKUTAMKIA BARAKA NA NEEMA KWENYE KILA UFANYACHO KWA KUMSHIRIKISHA MUNGU

Subscribe
Notify of
guest

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Msomaji

Amina

2
0
Tungependa maoni yako pia. Toa maonix
()
x